Mandojo kuzikwa leo saa 10 jioni

Mandojo kuzikwa leo saa 10 jioni

Mfanyabiashara na msanii Joseph Francis, maarufu Mandojo anatarajiwa kuzikwa leo Jumatano Agosti 14, 2024 saa 10 jioni wilayani Manyoni, Mkoa wa Singida.

Kutokana na ratiba iliyotolewa na familia ya marehemu, inaonyesha ibada itaanza saa 8 hadi saa 9.30 mchana kisha saa 10.30 jioni safari ya makaburini kwa ajili ya maziko itaanza.

Mandojo alifariki dunia Jumapili Agosti 11, 2024 saa 6.00 mchana, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, atazikwa leo Jumatano, Agosti 14, 2024 saa 10.00 jioni katika makaburi ya Kaloleni, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida ambako ndiko walikozikwa wazazi wake. Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.

Enzi za uhai wake aliwahi kutamba na ngoma kama vile Nikupe Nini, Dingi, Muziki Chacha na nyingine nyingi akiwa na mwanamuziki mwenzake Domo Kaya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags