Manara: Valentine siyo ya kila mtu

Manara: Valentine siyo ya kila mtu

Ikiwa leo ni sikukuu ya Wapendanao, aliyekuwa msemaji kwa ‘klabu’ ya yanga Haji Manara, ameeendeleza tambo zake katika siku hii ya leo na muda mchache uliopita ameachia ujumbe uliokuwa ukieleza kuwa sikukuu hiyo siyo ya kila mtu.

Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share picha akiwa na mkewe #Zaiylissa zilizoambatana na ujumbe uliokuwa ukieleza kuwa #Valentine siyo siku ya kila mtu wengine wasubiri sikukuu za Zimamoto au sikukuu za Mashujaa.

Hii ni posti ya pili kwa Manara kwa siku ya leo, ya kwanza ali-posti asubuhi akimtakia kheri ya siku ya valentine day mke wake huyo huku akiwazodoa watu ambao walisema ndoa yao haitafikia katika siku hiyo.

Manara na Zaiylissa walifunga ndoa Januari 24, mwaka huu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags