Manara amjibu Ahmed Ally

Manara amjibu Ahmed Ally

Aloooooh! Ama kweli mambo mengi muda ni mchache. Vita ni kali sana huko katika mitandao ya kijami kwa wasemaji hawa wawili na hii ni baada tu ya msemaji klabu ya simba Ahmed Ally kuandika ujumbe mrefu ukiwa unasema;

“Nchi nyingi za Afrika wanaitambua Simba kama miongoni mwa timu kubwa Afrika. Mchezaji akichezea Simba wanajua anacheza timu kubwa, anacheza mashindano makubwa na anapata experience kubwa. Timu nyingine za hapa Tanzania zinatambulika kuwa ni ndogo hata mchezaji anaecheza hapo anaonekana tu ni mdogo haijalishi anafunga usiku na mchana,” ameandika Ahmed Ally.

Maneno haya yamemtoka msemaji huyo baada ya timu ya taifa ya Congo kumchagua beki wa simba Enock Enonga ambapo swala hili lilizua mjadala kupitia mitandao ya kijamii ambapo watu walihoji kwanini Yanga hakuchaguliwa mchezaji hata mmoja licha kuwa wanafunga kila siku.

Basi bwana msemaji wa wananchi 'Yanga' hakukaa kimya kwa ujumbe huo ulioandikwa na Ahmed Ally na kufunguka kwa kusema kuwa, “Sawa mabingwa wa nchi Yanga Afrikaaaaaaa ni team ndogo kama ulivyotuambia ropokaji la Tadea, ndio uteleze hivyo kwenye bomba la watu? Huoni kwamba unaliumiza hilo bomba?, Bomba kama bomba, au basi,” ameandika Haji Manara.

Mmmmmmmh! Bado vita ni bila bila watu wangu wa nguvu. Vipi mnayapi ya kuwaambia wasemaji hawa wawili? Dondosha komenti yako hapo chini.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags