Man U watemana na Ronaldo

Man U watemana na Ronaldo

Club ya Manchester United imetangaza kumalizana na Staa wake Cristiano Ronaldo (37) kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Man United imemshukuru Ronaldo kwa utumishi wake wa vipindi viwili tofauti katika club hiyo “Cristiano Ronaldo anaondoka kwa makubaliano ya pande zote mbili, club inamshukuru kwa mchango wake wa vipindi viwili Old Trafford (2003-2009 & 2021-2022).

Mkataba wa Ronaldo na Manchester United ulikuwa unaisha mwisho wa msimu 2022/23 lakini inasemekana uhusiano wake mbaya na Kocha Erik Ten Hagen pamoja na interview yake na Piers Morgan vimechochea mkataba huo kuvunjika.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post