Man City yashusha presha kwa Haaland

Man City yashusha presha kwa Haaland

‘Klabu’ #ManchesterCity wana matumaini makubwa ya kuendelea kusalia na ‘straika’ wao #ErlingHaaland kwa muda mrefu zaidi baada ya  ‘klabu’ ya #RealMadrid kudaiwa kufikia makubaliano ya kumsajili mchezaji wa #PSG, #KylianMbappe.

Inaelezwa kuwa awali kulikuwa na tetesi kwamba Madrid ilikuwa imepanga kumchukua Haaland katika dirisha lijalo ikiwa ingemkosa Mbappe.

‘Staika’ huyo ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 baada ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Man City hivi karibuni ambapo ‘mabosi’ wa ‘timu’ hiyo walikuwa na wasiwasi wa kumpoteza.

Hata hivyo Madrid inapambana kusuka upya kikosi chao kwa kusajili mastaa wenye majina makubwa ambapo chaguo lao la kwanza lilikuwa ni Mbappe na la pili ni Haaland.

Mbappe anaonekana kuwa na asilimia zaidi ya 70 za kutua Madrid kwa sababu ameshawaambia ‘mabosi’ wa ‘klabu’ ya  #PSG kwamba ataondoka mwisho wa msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags