Mambo yatakayofanya uipende kazi yako

Mambo yatakayofanya uipende kazi yako

Na Aisha Lungato

Kuna uhusiano mkubwa kati ya furaha na utendani wako wa kazi, unapofurahia kazi yako unayofanya kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuzalisha zaidi kutokana na kuwa na uhusiano mzuri na kazi yako.

Moja ya sababu ya utendaji mbovu wa baadhi ya wafanyakazi kwenye taasisi mbalimbali ni kutoifurahia kazi , ukiachilia mbali mtu binafsi kujipa furaha pia mwajiri anaweza kuweka utaratibu mzuri utakaomwezesha mfanyakazi kuipenda kazi yake.

Kwa mfano siyo kila matatizo yanatokana na mtu binafsi kwani yapo yanayotokana na sehemu hisika ambayo inaweza kuchangia mfanyakazi kutoipenda kazi yake kama vile mazingira mabaya kazini, kutokuwa na vitu vya kumshawishi mfanyakazi.

Mwajiri kutoa motisha kwa wafanyakazi

Motisha inanafasi kubwa sana kwa mfanyakazi, itamfanya mfanyakazi wako kuwa na furaha na kuipenda kazi yake kwa hakika ni ngumu kuipenda kazi ambayo haina motisha.

Tunapozungumzia motisha siyo lazima iwe pesa vipo baadhi ya vitu vidogo ambavyo vinaweza kumfanya mtu kuipenda kazi yake kama vile, kutoa sabuni kila mwezi, sukari, kulipia mlo wa mchana wa kila mfanyakazi nk.

Kupenda wafanyakazi wenzako

Kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wenzio kutakufanya uwe na furaha wewe binafsi na kuipenda kazi yako, kuna mwandishi mmoja anayetambulika kwa jina la Christine Carter na kitabu chake cha The Sweet Spot: How to find your Groove at Home and Work’ kinaeleza kuwa “Katika kazi yoyote mahusino mazuri ni kiashiria namba moja na muhimu kitakachofanya kuwa na furaha ya kupitilia kazini”.

Hivyo basi jenga tabia ya kuwa karibu na wenzako, tafuta fursa za kushirikiana nao nje ya ofisi, pia tumia muda wako kubadilishana nao mawazo.

Kupata uhuru uwapo kazini

Binadamu kwa asilimia kubwa huwa anapenda sana kuwa huru katika mazingira yoyote yale na anaponyang’anywa uhuru wake ni kama umemnyang’anya furaha yake, kwa bahati mbaya zaidi baadhi ya kazi haziwapi uhuru wafanyakazi.

Hivyo basi mwajiri anayohaki ya kumpa mfayakazi wake uhuru wa kufanya jambo lolote isipokuwa lile litakaloharibu kazi pamoja na jina la taasisi husika.

Kujitambulisha kwa kazi yako

Siku zote mfanyakazi anajisikia fahari na furaha sana baada ya kuona kazi aliyofanya imeleta manufaa katika taasisi yake hivyo basi ili uweze kuifurahia na kuipenda kazi yako unatakiwa kujitoa katika kila unachokifanya ili kuleta matokea chanya katika taasisi yako.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags