Mama mzazi wa Costa Titch aapa kutafuta kilichomuua mwanae

Mama mzazi wa Costa Titch aapa kutafuta kilichomuua mwanae

Mama Mzazi wa Costa Titch jana kupitia ukurasa wa Instagram wa marehemu mwanae ameeleza kwamba hatatulia au kuishi kwa furaha na amani mpaka hapo atakapofahamu ni sababu gani iliyopelekea kifo cha mtoto wake huyo.

Kupitia ukurasa huo aliandika kuwa “I promise you my son, that I will not rest until I find out what happened to you” ameandika Mama Costa Titch.



Mbali na kuahidi kufatilia chanzo cha kifo cha Mwanae, mwanamama huyo pia katika post nyingine ameeleza namna gani anavyojivunia mtoto wake

Ikumbukwe tu Costa Titch alifariki March 11 2023 Johannesburg, South Africa wakati akitumbuiza kwenye jukwaa la Ultra South Africa Music Festival.

Mpaka sasa chanzo halisi cha kifo chake hakijawekwa wazi ingawa kuna watu wengi wanadai kwamba kwa muda mrefu alikuwa ana tatizo la kifafa hivyo huenda ndio ugonjwa uliopelekea aanguke jukwaani na kufariki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags