Majeraha ya wachezaji yampa hofu kocha wa Chelsea

Majeraha ya wachezaji yampa hofu kocha wa Chelsea

Taarifa zinaeleza kuwa star mpya aliyesajiliwa na ‘klabu’ ya #Chelsea, #RomeoLavia ameumia kifundo cha mguu wakati wa mazoezi week iliyopita huku Carney Chukwuemeka naye akipata majeraha.

Kutokana na hayo inadaiwa kuwa ‘Kocha’ wa ‘timu’ hiyo, Mauricio Pochettino ameingiwa na hofu baada ya wachezaji wake muhimu kupata majeraha na atawakosa katika ‘mechi’ ijayo ya ‘ligi’ dhidi ya #Bournemouth.

Ingawa Lavia hakujumuishwa kwenye kikosi tangu aliposajiliwa kwa Pauni 58 milioni kutoka #Southampton ikidaiwa kwamba bado hakuwa ‘fiti’ asilimia 100. Pochettino aliweka wazi kuwa kiungo huyo atakuwa ‘fiti’ baada ya ‘mechi’ za kimataifa lakini  kutokana majeraha aliyopata huenda akaongezewa muda zaidi wa kukaa nje bila kucheza.

Hata hivyo Pochettino amepata pigo jingine baada ya nyota wake mwingine Chukwuemeka kuumia na huenda akawa nje ya dimba kwa muda mrefu.

Inadaiwa kuwa Chukwuemeka atakuwa nje kwa muda wa week sita baada ya kuumia katika ‘mechi’ ya ‘Ligi’ kuu ya #England dhidi ya #WestHam kiungo huyo aliyetarajiwa kurejea uwanjani kwa kipindi hichi lakini mambo yamekuwa tofauti.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags