Mahakama  yasitisha tarehe ya mwisho kubadilisha noti

Mahakama yasitisha tarehe ya mwisho kubadilisha noti

Mahakama ya Juu nchini Nigeria imesitisha kwa muda shauri la kuacha kutumia noti za zamani, jambo ambalo lilikuwa limesababisha mzozo wa fedha nchini humo.

Benki nyingi hazijapata noti mpya za naira za kutosha, na kusababisha matukio ya kukata tamaa na machafuko huku watu wakijaribu kuzipata na wengine wakivua nguo kwenye benki katika maandamano na mapigano kwenye ATM.

Machafuko hayo yalisababisha wasiwasi kuwa huenda yakaathiri uchaguzi wa mwezi huu, kwani Wanigeria wengi hawana akaunti za benki.

Benki Kuu ilitangaza sarafu iliyobuniwa upya katika jaribio la kudhibiti mfumuko wa bei, ambao kwa sasa unaendelea kwa 20%.

Aidha kesi hiyo iliyoletwa na majimbo ya kaskazini ya Kaduna, Kogi na Zamfara imeahirishwa hadi Februari 15.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags