Magauni yenye gharama zaidi duniani lipo la 77 bilioni

Magauni yenye gharama zaidi duniani lipo la 77 bilioni

Haya ndiyo magauni yenye gharama zaidi duniani. Vipi unaweza kununua au tukuache na nguo zako za kariakoo?

1.Nightingale ya Kuala Lumpur yenye gharama ya dola 30 milioni sawa na Sh 77.3 bilioni

Nguo ghali zaidi ambayo mpaka leo hakuna wa kuipiku ni gauni la Nightingale ya Kuala Lumpur lililotengenezwa na Faisal Abdullah mwaka 2009, limetengenezwa kwa kutumia hariri nyekundu pamoja na zaidi ya almasi 750.

2.The Abaya Dress kutoka kwa Debbie Wingham lenye gharama ya dola 17.7 milioni sawa na Sh 45.6 bilioni

Hii ndiyo nguo namba mbili yenye gharama zaidi iliyotengenezwa na mbunifu kutoka nchini Uingereza Debbie Wingham. Gauni hili 'limedizainiwa' kwa almasi zaidi ya 2000.

3.Hany El Behairy  Dress lenye gharama ya dola 15 milioni sawa na Sh 38.6 bilioni.

Gauni jingine ambalo lipo kwenye orodha ya nguo zenye gharama zaidi ni gauni lililotengenezwa na mbunifu wa mavazi kutoka Misri aitwaye Hany El Behairy, lilitengenezwa kwa ajili ya harusi ya familia tajiri kutoka Misri likichukua zaidi ya saa 800 kukamilika, lilipambwa kwa mamia ya almasi pamoja na vito vya thamani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags