Madrid yagoma kumtoa Arda Guler

Madrid yagoma kumtoa Arda Guler

‘Klabu’ ya #RealMadrid imekataa ofa kwa ‘klabu’ zinazomuhitaji mchezaji wao Arda Guler, wakisisitiza kuwa bado wanamatumizi naye hivyo hataruhusiwa kuondoka klabuni hapo mpaka mkataba wake utakapoisha.

Kwa mujibu wa Sky Sport imeeleza kuwa kiungo huyo mshambuliaji ameendelea kushiliwa na timu hiyo kutokana na ubora wake licha ya klabu mbalimbali kumtaka ikiwemo AC Milan na Barcelona.

Hata hivyo kwa upande wake Guler amedai kuwa hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo na ameielekeza akili yake katika mashindano ya Euro 2024 akiwa na ‘timu’ ya taifa ya Uturuki.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 raia wa Uturuki, alijiunga na kikosi hicho mwaka jana kwa mkataba wa miaka sita klabuni hapo hadi mwaka 2029.

Kiungo huyo amechangia katika kikosi hicho kupata kombe katika fainal Supercopa Januari 14,2024 ambapo Madrid ilishinda mabao 4-1 dhidi ya klabu ya Barcelona. Aidha Aprili 26 alianza kucheza ‘La Liga’ na kuipa timu yake ushindi wa 1-0 dhidi ya Real Sociedad.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags