Madonna aweka rekodi kufanya show mbele ya mashabiki milioni 1.6

Madonna aweka rekodi kufanya show mbele ya mashabiki milioni 1.6

Mkongwe wa muziki wa Pop, nchini Marekani Madonna ameweka rekodi kwa kuandaa tamasha kubwa kwenye ufukwe wa Copacabana katika mji wa Rio de Janeiro, Brazili siku ya Jumamosi.

Kwa mujibu wa tovuti ya Time News imeeleza kuwa onesho hilo ambalo msanii huyo alilifanya bila kiingilo chochote kwa mashabiki wake, lilivuta idadi kubwa ya mashabiki hadi kufikia jumla ya watu milioni 1.6, walihudhuria katika tamasha hilo.

Tamasha hilo lilikuwa la mwisho katika ziara yake ya ‘The Celebration Tour’, ambayo ilianza London nchini Uingereza Oktoba, 2023 ambapo pia alipokelewa na umati mkubwa, hali iliyomfanya abaki kimya kwa muda wa dakika moja.

Onesho hilo limekuwa zaidi ya mara 10 ya rekodi yake ya awali ya watu 130,000 aliyoifanya msanii huyo mkongwe, Paris mwaka 1987.

Madonna aliweza kutumbuiza vibao vyake vya zamani katika tamasha hilo vikiwemo Like A Virgin, na Hung Up ikiwa ni moja ya utangulizi wake.

Licha ya kuwa na watu wengi katika tamasha hilo lakini usalama wa eneo hilo uliimarishwa na wanajeshi 3,200 na maafisa wa polisi 1,500 waliosimamia ulinzi kabla ya tamasha hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags