Madonna ajibu kesi ya kuchelewa kwenye matamasha yake

Madonna ajibu kesi ya kuchelewa kwenye matamasha yake

Mwanamuziki wa Marekani Madonna amejibu kesi iliyokuwa ikimkabili ya kuchelewa kuanza kwa matamasha yake.

Kwa mujibu wa nyaraka kutoka Mahakamani zilizochapishwa na Tmz Madonna alieleza kuwa mashabiki wake wa kweli wanatambua muda wake wa kuingia jukwaani hivyo basi tuhuma hizo siyo za kweli huku timu ya wanasheria wa Madonna ikiomba kesi hiyo itupiliwe mbali.

“Ikiwa shabiki anaifahamu vya kutosha historia ya tamasha la Madonna kujua maonesho yake yanaendeshwa kwa saa mbili na dakika kumi na tano, shabiki huyo bila shaka atajua kwamba Madonna kwa kawaida hupanda jukwaani vizuri baada ya muda wa tukio uliyopo kwenye tiketi”

Ikumbukwe kuwa Januari 2024 mashabiki wawili wa Madonna waliotambulika kwa majina Michael Fellows na Jonathan Hadden, walimfungulia mashitaka msanii huyo kwa kuchelewa kupanda jukwaani kwa zaidi ya saa mbili katika tamasha lake la 13 Desemba 2023.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post