Madhara ya matumizi mabaya ya simu

Madhara ya matumizi mabaya ya simu

Ni wiki nyingine tena tukikutana katika safu ya teknolojia kujuzana marefu na mapana. Despite the vivid growth of technology is the digital era, ukweli ni kwamba madhara yanaenda sambamba na faida, hivyo ni vizuri mara moja moja kukumbushana juu ya implications of technology.

In the recent months, tumeona wasichana wengi sana ambao ni vijana wakidhalilika au kudhalilishwa mitandaoni kwa kuvuja video zao za utupu. Hii ni moja kati ya mfano tu wa madhara ya utandawazi.

Katika dunia ya sasa, hasa kwa mwanachuo kama wewe, nina amini kuwa una simu janja yaani smartphone. Your phone can be the greatest assest you could own as a university student! Faida kama vile mawasiliano rahisi na marafiki, ndugu na jamaa, kuweza kujisomea material mtandaoni, pamoja na kujua kama mwalimu ametoa coursework, ni sababu chache tu ya kwanini uwe na smartphone.

 Lakini je, unajua kuwa simu pia inaweza kukugeukia na kukuletea maafa makubwa? It all depends on how you decide to use that equipement and it will either make you or break you!

Anyway, lets dive into the negative effects of misusing your cellphone.

  1. Simu inaweza 'kubadilisha tabia yako kijamii'

Kuna ushahidi wa wazi ambao wanasaikolojia wanasema matumizi ya simu yanaweza kuleta kwa tabia ya mtu hasa kijamii .

Sio jambo la ajabu kujua kwamba kwa sasa kuna watu hasa vijana ambao matumizi ya simu yameathiri sana uwezo wao hata kuweza kutangamana kwa njia ya kawaida.

  1. Kutumia simu ukiendesha gari au ukifanya kazi inayohitaji umakinifu

Umeskia kuhusu ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva ambao wanaendesha gari wakitumia simu za mkononi

Takwimu ni nyingi kuhusu idadi ya maafa yanayosababishwa na ajali kama hizo .

Kumekuwa na kampeni kote duniani na hasa kutoka kwa polisi kuhusu hatari ya kuendesha gari ukitumia simu .

  1. Umetumiwa pesa kwenye simu ukazitoa na sio zako?

Umeyaskia hayo kuhusu watu kuzitumia simu vibaya kwa kutoa fedha wanazotumiwa kimakosa .

Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakitumia simu kama kinga ya kufanya maovu na uhalifu .Sheria zinabadilika na kuboreshwa na usije ukadanganyika kwamba unaweza kutekeleza uhalifu kutumia simu yako ukifikiri uko salama.

  1. Hakikisha unanunua simu yako kwa njia halali ama kwa muuzaji mwenye leseni

Iwapo ulifikiri unaweza kuinunua simu ya mkononi kwa yeyote kwa sababu umeipata kwa gharama ya chini ,basi itabidi umeliwazia tena suala hilo . Kuna hatari kubwa sana kununua simu kutoka kwa mtu yeyote.

Kunayo mifano ya watu waliofungwa jela kwa makosa makubwa hata ya mauaji kwa kuuziwa simu ambazo zilipatikana kupitia uhalifu .

  1. Matumizi ya simu yaliyokithiri husababisha kuwa wapenzi wengi miongoni mwa wanafunzi 

Haya sio maneno yangu, huu ni utafiti uliofanyika Katika utafiti wa zaidi ya watu 3,400 nchini Marekani wanaosoma shahada ya kwanza.

Kwa hao wenye matumizi yaliyozidi ya simu za mkononi, wameripotiwa pia na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya mwenza mmoja katika kipindi cha miezi 12, kuliko wale waliokutwa hawana matumizi makubwa ya simu.

Sasa kama hizo sababu hapo juu hazitoshi, usiseme sikukushauri kutumia simu yako vizuri. Hakikisha your smartphone inakujenga na sio kukubomoa, hivyo basi hata maisha yako yatakwenda sawia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags