Madhara ya kuvaa Viatu virefu

Madhara ya kuvaa Viatu virefu

Niaje, wanangu!Leo katika urembo na fashion utaweza kujifunza kuhusu madhara ya kuvaa mchuchumio’ ama viatu vyenye  visigino virefu.

Viatu virefu ni mojawapo ya vitu vinavyopendwa na baadhi ya wanawake mbalimbali, sio Tanzania pekee bali dunia nzima.

Wataalamu wanaeleza kuwa viatu hivi huharibu pingili za uti wa mgongo na huvunjavunja mifupa ya visigino. Wanawake wenye maumbo ya kati, ambao si wanene wala wembamba wamekuwa wakipendelea viatu virefu. Kwa kiasi kikubwa wasichana wafupi, wamekuwa wakipendelea kuvaa viatu virefu ili angalau na wao waonekane warefu.

Ifahamike kuwa unapovaa viatu hivi uzito wako huhamia mbele ya mwili na kufanya nyonga isogee mbele na kumfanya mtu awe na kiuno kizuri na mgongo unaovutia hivyo kutegemea viatu hivi kwa muda huharibu umbo pale anapovaa viatu vya kawaida.

 

Misuli ya visigino kukakamaa na kumfanya mtu aonekane na mguu mzuri ufunga vidole vya miguu na kusababisha maumivu makali chini ya mgongo. na ulemavu wa vidole. Pia uweza kusababisha ugonjwa wa arthritisi kadiri umri unavyoongezeka na matatizo ya uzazi katika nyonga kutokana na kuelemewa na uzito asa kwenye jointi za magoti na nyonga.

ILI KUEPUKA MADHARA HAYA ZINGATIA YAFUATAYO

Fanya mazoezi ya kunyoosha miguu kabla ya kuvaa viatu hivi.


Vaa viatu virefu kiasi maana kila urefu unavyoongezeka, madhara yake huongezeka pia.

Nunua viatu hivi wakati wa mchana ,mguu wako unakuwa umetanuka kidogo hivyo utaweza kupata size inayokufaa.

Usivae viatu virefu vilivyochongoka upande wa kidole gumba tu.


Vaa viatu vyenye ngozi kwa ndani ili kuwezesha miguu kukaa vizuri.


Kuwa na pea nyingi za viatu ili kukuwezesha kubadilisha inapotokea madhara.


Usivae sana wakati unatembea mwendo mrefu, wa haraka, na unatumia usafiri wa umma.

 






Comments 1


  • Awesome Image
    Innocent kapinga

    Bless sana bibie kuruthum tupo pamoja ... Never give up... Tuambie location wapi

Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags