Madhara ya kutumia muda mwingi kufanya mambo yasiofaa kazini

Madhara ya kutumia muda mwingi kufanya mambo yasiofaa kazini

Mamboz!! Once again tunakutana on this weekend wanetu wa faida kwenye hii sgment yetu ya maswala ya kazi, hapa tunawekana sawa kuhusiana na mambo mbalimbali ya kazi.

Wiki iliopita tulizungumza ufanyaji wakazi za vibarua unaonekane katika jamii tukaona mambo yanayo hatarisha kazi za vibarua na changamoto wanazukumbana nazo.

Leo katika kipengele cha kazi tumekusogezea madhara ya kutumia muda mwingi kufanya mambo yasiofaa kazini.

Ni hatari sana kuleta mambo ambayo ya kusababishia pengine hata kukosa kazi najua kuna watu wao wakifika kazini wameona ndio kama sehemu ya kupiga soga (umbea) ambazo haziusiania na kazi, ili mradi tu apoteze muda kumbuka hapo muda haurudi nyuma mwamba.

Pia kuingia mtandaoni kuaangalia habari za udaku wakati masaa ya kufanya kazi unayapoteza kwa vitu visivyo na msingi mtandaoni, unakuta mtu kafika kazini kitu cha kwanza anachukua simu yake na kuperuzi mtandao bila kujali sehemu ya kazi.

Kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi mwenzio yaani hapa ndio unapoteza kabisa kwasababu ukifanya hivyo utapoteza ufanisi wakazi na uzembe wa hali ya juu hautafikiria maswala ya kazi zaidi ya mpenzi wako.

Kutumia muda mwingi kupata breakfast na lunch yaan unakuwa unatumia muda mwingi kula kuliko kufanya kazi ukifika ofisini unawaza kula badala ya kazi unakuta una maliza masaa mawili kwa kula tu bila kuzingatia kazi za watu ofisini tena hii ni moja ya dalili ya uvivu.

Tuje sasa kwenye point yenyewe madhara ya kufanya mambo yasio faa kazini.

  • KUKOSA UFANISI KATIKA KAZI

Lazima ukose ufanisi waufanyaji kazi ukiendekeza ujinga kazini hakuna ambae ameshawahi kufanya uzembe kazini na akafanikiwa yaani hata dunia ibadilike iko hivyo mtu yeyote duniani ukisia anaufanisi katika jambo Fulani ujue hakufanyaga uzembe juu ya hicho kitu hususani maswala ya kazi.

  • KUSHUSHWA CHEO KAZINI

Yaani hii ndio haichelewi tena kwa maboss ambao wako serious wanafatilia kila nukta yako sasa kama umepewa cheo usimamie kitu Fulani na pengine umeleta maswala ya mapenzi na ikagundulika au jambo lolote lkakushushia cv yako mwamba cheo hapo hauna. So chakufanya inabidi ubadilike ili uwe bora.

  • KUTOSIKILIZWA KAZINI

Sasa umeshaonekana hauna unachokifanya kazi yaani hauna maana hauwezi ukasilizwa na mtu yeyote ofisini na ndio mwanzo wa kutoshirikishwa kwajambo lolote na kuweka katika danger zone yaani muda wowote ofisi ikiamua inakutimua.

  • KUPUNGUZIWA MSHAHARA AU MSHARA KUFUTWA KABISA

Hapa unakuwa hauna ambalo ofisi wanajivunia kupitia wewe ambacho kita kufanya uwashawishi kuongezewa mshahara au mshahara uwe kama siku zote mimi nasemaga kama una malengo basi sidhani kama uta fanya uzembe wowote kazi.

  • KUFUKUZWA KAZI PASIPO KUPEWA TAARIFA

Yaani wamekuchoka kazini kutokana na tabia yako mbaya labda ya kuendekeza uvivu au kufanya umbea kugombanisha watu utajikuta unapewa bahasha yako na neno utakaloliskia kutoka kwa bossi wako “nenda home mpaka tutakapo kuhitaji tutakupigia simu” kama ulikuwa haujui ukishaskia kauli hii basi tafuta jambo linguine la kufanya yaani ujiongeze.

Jambo muhumu la kuzingatia mwanetu hakikisha unapokuwa ofisini au katika kazi yoyote nidhamu ya kazi muhimu kwasababu itakuongezea credit ya kutoka kwenye zero mpaka kwenye mia hapo mambo yanakuwa mswano kabisa.

Heshimu kazi na uipende kazi yako kwa hali yoyote hiyo kazi ni sehemu ya kutengeneza future yako ya maisha labda itokee haufanyi kazi kwa malengo hapa wananielewa wenye malengo yao kazini wananielewa na maanisha nini.

Sasa wewe mwamba unaefanya uzembe saivi kazini nikwambie tu kuna wana wapo tu mtaani wananidhamu na kazi na wanatafuta kwa udi na uvumba na uhakika wa kupata kazi watafanya mambo makubwa

Kwaushauri sahihisha makosa upambane hali ngumu mjomba na kumbuka kila kitu kina muda wake baki na maneno haya “Fanya kazi fainali uzeeni” sisi Team Scoop utakuja kutushukuru badae tupo tumekaa pale .

 

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post