Madam Rita: Sina mume wala mchumba, Nahisi wananiogopa

Madam Rita: Sina mume wala mchumba, Nahisi wananiogopa

Mkurugenzi wa Bongo Star Search #BSS, #RitaPaulsen maarufu kama Madam Rita, amedai kuwa hana mume wala mchumba anahisi wanaume wanamuogopa.

Akizungumza na moja ya chombo cha habari nchini madam Rita amesema kuwa hayupo kwenye mahusiano na anahisi wanaume wanaogopa kumfata, japo aliwahi kuwa kwenye mahusiano kipindi cha nyuma lakini kwa sasa haijawahi kutokea mwanaume kumwambia anampenda.

Hata hivyo Rita ambaye ana mtoto mmoja amesema kuwa kama akitokea mwanaume akampenda basi atakuwa naye kwa sababu hajaolewa na hakuna mtu wa kumzuia kuwa kwenye mahusiano.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags