Mackenzie atazeekea gerezani, Kindiki

Mackenzie atazeekea gerezani, Kindiki

Sakata la Mchungaji Paul Mackenzie raia wa Kenya limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Usalama wa ndani nchini humo, Kithure Kindiki kusema kuwa hatoachiwa huru na badala yake atazeekea jela akidai kuwa ameua watu wengi zaidi kuliko magaidi walioua katika miaka 10.

Mchungaji huyo ambaye anadaiwa kumiliki msitu wa Shakahola anachunguzwa kwa kushawishi waumini wake wa Kanisa la Good News International kufa njaa kwa ahadi ya kukutana na Yesu.

Mhubiri huyo ameendelea kusisitiza kwamba hana makosa na kuwa amezuiliwa kinyume cha sheria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags