Mabosi  yanga waweka mkwanja Belouizdad apasuke

Mabosi yanga waweka mkwanja Belouizdad apasuke

Matajiri wa Yanga jana usiku walikutana na wachezaji kuwapa ahadi nzito ya fedha isiyopungua Sh500 milioni kwa ushindi, lakini kabla ya hapo kambini kwa wachezaji kumekuwa na mzuka mkubwa.

Yanga wamejidhatiti kuhakikisha safari hii wanacheza robo fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi ngazi ya ‘klabu’ Afrika baada ya msimu uliopita kucheza fainali za Kombe la Shirikisho na kukosa ubingwa kikanuni.

Yanga itaingia kibaruani siku ya leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Belouizdad, ‘mechi’ itakayocheza Saa 1:00 usiku.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags