Mabeste Afunga Ndoa

Mabeste Afunga Ndoa

Rapa na mtayarishaji wa muziki nchini , Mabeste amefunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Divashia.

Mabeste ameweka wazi taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram akionyesha furaha yake kwa kufunga ndoa na mpenzi wake.

"Hatimaye, subira imezaa heri! Nimebarikiwa kufunga ndoa na mwanamke mrembo, mwenye akili, na mwenye upendo wa dhati. Safari imekuwa ya thamani kila hatua," ameandika Mabeste.

Utakumbuka, hii inakuwa ndoa ya pili kwa rapa huyo baada ya kuachana na mke wake wa kwanza Lisah Karl mwaka 2019 ambaye walibahatika kupata watoto wawili, Kendrick na Catelyn Mabeste.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags