Maarifa ajipanga kuitumia kumbukizi ya kifo cha mama yake kurudi kwa mashabiki

Maarifa ajipanga kuitumia kumbukizi ya kifo cha mama yake kurudi kwa mashabiki

Baada ya ukimya wa takribani mwaka mmoja kwenye muziki, rapa Rashid Rais maarufu Maarifa Big Thinker amefunguka kuja na zawadi kwa mashabiki wake.

Zawadi hiyo ambayo ni wimbo mpya atautoa siku ya kumbukizi ya kifo cha mama yake na kumbukizi ya kuzaliwa kwake Julai 22 mwaka huu.

“Watu wakae mkao wa kula, Julai 22 nitatoa kibao changu cha sita siku hiyo ambayo itakuwa ni kumbukizi ya kifo cha mama yangu aliyefariki mwaka 2003 na siku yangu ya kuzaliwa,” amesema.

Hata hivyo ameeleza lengo la kutoa wimbo katika siku hiyo ni kumbukumbu katika maisha yake.

“Kwa nini nimechagua tarehe hiyo ni kwa sababu hizo ni kumbukumbu kubwa sana kwangu lakini kwa upande mwingine nimekaa mwaka mmoja na miezi sita bila kutoa wimbo wowote, nimeona niongeze kitu kingine cha tatu kwenye hiyo kumbukumbu kwa kuwapa watu kitu ambacho walikuwa wanakisubiri kwa muda mrefu,” amesema.

Pia Maarifa ameeleza sababu ya ukimya wake akidai kuna wakati maudhui peke yake hayatoshi kumburudisha shabiki.

“Kwenye muziki kunahitaji mabadiliko na utofauti kwa sababu kuna muda kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja haimaanishi watu hawatokuchoka, ifike mahali wasanii wajue kuwa maudhui peke yake hayatoshi kumburudisha shabiki hata ladha ya nyimbo pia inachangia ndiyo maana mimi tangu nimeanza muziki mpaka sasa nina nyimbo tano tu,” amesema Maarifa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post