Maajabu ya ulimi wa Simba

Maajabu ya ulimi wa Simba

Moja kati ya viungo muhimu kwenye mwili wa mnyama Simba ni ulimi wake ambao anautumia kwa namna nyingi, ulimi huo humrahisishia mambo mengi ambayo humuwezesha kuendelea kuishi.

Simba hutumia ulimi wake kulamba ngozi ya mnyama au chakula ambacho anataka kula ili kuondoa manyoya, kwa sababu ulimi wake una miba mikali kama msasa wa kusugulia ukuta.

Hivyo kabla ya kula ni lazima alambe chakula husika kwa muda mrefu, na kufanya chakula kiende kumeng'enywa vizuri, pia hutumia katika kunywa maji, ambapo kwa kawaida hunywa kwa kulamba.

Hata hivyo kutokana na maeneo ambayo wanapatikana kuwa na joto sana, Simba hutumia ndimi zao kulambana wakiwa na ishara mbili, kwanza ni kupunguza joto kupitia mate ambayo hugusa ngozi, pia kwao kulambana ni ishara ya upendo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags