Moja kati ya wanyama wafugwao majumbani ni paka, huku wengine wakiwatumia kwa ajili ya kumaliza panya na wengine huwafuga kwa kupenda tu.
Kati ya vitu ambavyo humpa paka muonekano wa kipekee ni macho yake yenye kung'aa, manyoya pamoja na sharubu, inaelezwa kuwa kati ya vitu muhimu kwa mnyama huyu ni sharubu zake ambazo zipo 24 hukaa 12 kwenye upande wa kushoto na nyingine kulia.
Sharubu hizo paka huzitumia kama futi ya kupima, yaani umewahi kuona paka akipita kwenye tobo dogo na ukajiuliza kawezake, basi kabla ya kupita huweka kwanza kichwa chake ili kupima kupitia sharubu zake ambazo humjulisha kama anapita ama hapiti.
Kwa kutumia sharubu huweza kutembea usiku kwenye giza kali kwani zinauwezo wa kumjulisha sehemu zenye vikwazo za kutopita.
Pia hutumika kama sehemu ya kulinda uso wake na macho yake kwani sharubu hizo ndiyo huwa za kwanza kupata hisia ya kitu chochote kinachokaribia uso mwake.
Sharubu za paka zimeunganishwa na tishu zenye neva nyingi za fahamu. Neva hizo zinauwezo mkubwa wa kutambua hata msukumo mdogo wa hewa, pia anazitumia sharubu zake katika kujua mahali na mwendo wa windo au kitu fulani.
Kimsingi sharubu ndiyo maisha ya Paka ikiwa zitakatwa, huenda asichukue muda mrefu akapoteza maisha.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply