Maajabu wa Tango katika kupambana na maradhi

Maajabu wa Tango katika kupambana na maradhi

Siku zote mwili wa binadamu ili uweze kuwa katika afya nzuri unahitaji virutubisho mbalimbali ambavyo vinapatikana katika vyakula tunavyokula kila siku.

Pale mwili unapokosa virutisho hivyo basi usababisha mwili kuwa dhaifu kiafya(kumbuka mwili haujengwi na matofali).

Tango ni tunda mojawapo ambalo linafahamika sasa na ni moja ya tunda lenye virutubisho vingi sana ambayo uwezesha mwili kuwa na afya njema.

Tunda hili ni chanzo kizuri cha Kashiamu, Chuma, Vitamini C, Phosforas, Potasiamu, Zinki, Kambalishe, Vitamini B complex na Vitamin E.

Unapojua umuhimu wa kitu inakuwa ni rahisi sana kuanza kuchukua uamuzi na kufanyia kazi.Vivyo hivyo katika swala zima  la virutubisho katika mwili wako, pale unapojua umuhimu wa kula tunda fulani  na faida zake katika afya ya mwili wako, utachukua uamuzi wa kuanza kulila mara kwa mara.

Kabla sijakupa faida za tunda la Tango ningependa ufahamu hili ya kuwa kujua umihimu au faida za kula matunda ni tofauti na mtu aliyechukua hatua ya kuanza kula matunda mara kwa mara.

Watu wengi wanafahamu umuhimu wa kula matunda lakini sio wote waliochukua hatua ya kula matunda mbalimbali hata kama yanapatikana kwa urahisi.

Nategemea msomaji wangu wewe utakuwa wa tofauti unapojua faida za kula matunda ni vyema ukaanza kula mara kwa mara.

Miongoni mwa faida za tango kiafya ni kama zifuatazo

Husaidia mmeng'enyo wa chakula mwilini

Kwa mujibu wa wataalamu wa sayansi ya afya, wanasema Tango husifika katika kusaidia katika mmeng'enyo wa chakula na pia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa erepsin enzyme.

Kutokana na umuhimu huo watu wanashauriwa kutumia tango ama liwe katika mfumo wa juisi kama baadhi wanavyotengeneza kula likiwa bichi au kukatakata vipande kisha kutafuna.

Upunguza hatari ya kupata kansa na saratani

Tango husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa kwa sababu zina kiwango kikubwa cha virutubisho viitavyo lignas ambavyo husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili.

Kula tango mara kwa mara humsaidia mlaji kujikinga dhidi ya saratani za aina mbalimbali,tango lina kiwango kikubwa cha  uchachu(alkaline) ambacho huzuia seli za saratani kuishi kwani haziwezi kuishi kwenye mazingira ya uchachu.

Huongeza Vitamin C mwilini

Tango linakiwango kikubwa na vitamini C ambayo husaidia kuondoa matatizo mbalimbali yanayosababishwa na ukosefu wa vitamin C kama vile kuota meno na mifupa vibaya pia kutokwa na damu kwenye fizi.

Kupunguza uzito

Kama unazuito uliyokithiri basi tango linaweza kuwa moja ya tiba ya kuuondoa uzito huo na ukawa mtu mwenye afya njema kabisaa.

Tango kama yalivyo matunda mengine ina virutubisho vingi ambavyo husaidia kupunguza uzito katika mwili na hiyo ni kutokan ana kuwa na ‘kalori’ chache.

Huboresha kiwango cha maji mwilini

Mwili wa binadamu unahitaji kuwa na maji muda wote, pale mwili wako unapokosa kuwa na maji afya ya mwili wako ipo hatarini.

Ulaji wa matango usaidia kuboresha kiwango cha maji mwilini ambayo husaidia kuondoa taka mwilini na sumu zilizopatikana katika ulaji wa vyakula mbalimbali.

Kwa mujibu wa gazeti la afya ‘Healthline’ limebainisha kuwa ulaji wa matunda na mboga huchangia asilimia 40 ya maji mwilini, Utafiti wao unaonesha kuwa tango pia lina asilimia 96 ya maji huku asilimia zilizobakia zikiwa na vitamin na viinilishe.

Huondoa harufu mbaya kinywani

Kwa wale wanaosumbuliwa na kuwa na harufu mbaya kinywani wanashauriw kula matango mara kwa mara kwa sababu huweza kuua bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya kinywani.

Ni tiba ya hangover

Kwa wale wanaosumbuliwa na hangover au kichwa kuuma nyakati za asubuhi,wanashauriwa kula tango kabla ya kwenda kulala,matango yana vitamini B  na electrolyte ambayo husaidia kuondoa hali ya hangover.

Najua mpenzi wa mwananchi Scoop utakuwa umejifunza mengi kupitia Makala hii usikose kutufatilia tena katika dondoo za afya wiki ijayo.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post