Maajabu 10 ya Nyangumi

Maajabu 10 ya Nyangumi

Unaambiwa kuwa inasadikika Nyangumi ndie kiumbe mkubwa duniani kiote.

Basi nimekusogezea maajabu 10 ya kiumbe huyo wa ajabuy.

  1. Moyo wa nyangumi una kilo 600, ukubwa wake ni sawa sawa na ukubwa wa gari ndogo.
  2. Mtoto wa Nyangumi akifikisha miezi 7 ana kunywa maji sio chini ya lita400 kwa Siku
  3. Mtoto wa Nyangumi ana uzito wa kilo2700 ni sawasawa na mnyama Kifaru mkubwa.
  4. Uzito wa nyangumi mkubwa unakadiriwa kuwa wa tani 200 hadi 300
  5. Ulimi wa Nyangumi mkubwa una uzito wa tani3 ni zaidi ya uzito wa tembo mkubwa

6 .Mdomo wa nyangumi unaweza kuhifazi tani 90 za chakula na maji akiufumbua mpaka mwisho

  1. Nyangumi anaweza kuishi mpaka kufikia miaka 80
  2. Chakula kikuu cha nyangumi ni dagaa kamba, ambapo nyangumi mkubwa hula dagaa kamba zaidi ya 4,000,000 kwa siku, ili nyangumi ashibe vizuri anakula kilo 3600kg
  3. Urefu wa nyangumi unakadiriwa kuwa wa mita 30 mpaka 50, ukimuweka ardhini urefu wake ni sawa sawa na urefu utakao jitokeza baada ya kuyapanga magari 9 ya ukubwa wa Noah.

Aliyekamatwa mara ya mwisho alikuwa na urefu wa mita 33.

  1. Cha kustaajabisha Nyangumi ndio mnyama mwenye sauti kubwa kuliko kitu chochote duniani.

Hutoa sauti kali sana ya kipimo cha Decibles 188 ambayo inaweza kusikika mpaka umbali wa kilomita 848.

Ni sauti kubwa na kali kuliko sauti itoayo ndege kubwa aina ya jet inapo paa ambayo kipimo cha sauti ya jet ni decibles 120.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags