Maafisa kuchunguza waliomfananisha Lebron na Tumbili

Maafisa kuchunguza waliomfananisha Lebron na Tumbili

Maafisa elimu Marekani wameingi katika uchunguzi wa bango la ubaguzi wa rangi lililomlinganisha nyota wa NBA, LeBron James na tumbili katika tangazo la chakula cha nafaka liitwalo ‘Monkey Premium’.

Tangazo hilo ambalo lilifanywa na wanafunzi wa shule ya ‘New Hartford Central School District’ iliyopo jijini New York lilifananishwa na alilolifanya LeBron katika chapa ya ‘Eat Monkeys, Jump Like Monkeys’.

Hata hivyo kufuatiwa na suala hilo mkuu wa shule hiyo Dk. Tangorra Jr alitoa neno siku ya jana Alhamisi kupitia WIBX kwa kusema kuwa mwanafunzi hawakuwa na hatia yoyote bali ni mwalimu ambaye alikubali tangazo hilo lifanywe na wanafunzi.

Aidha Mkuu huyo aliwaomba radhi wale wote walioguswa na suala hili huku akiahidi kuwa mtuhumiwa atafikisha katika sehemu husika za sheria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags