Kila Januari 4 ya kila Mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Nukta Nundu kwa lengo la kuongeza Ufahamu kuhusu haki za binadamu kwa wenye Ulemavu wa Kuona, na Uoni Hafifu.
Madhumuni ya Siku hii ni kuhamasisha Umma kuhusu thamani ya ‘Nukta Nundu” kama njia ya Mawasiliano kwa Wenye Ulemavu wa Kuona
Aidha Nukta Nundu (Braille) ni Kiwakilishi cha kugusa chenye Alama za Namba na Alfabeti, ambapo Herufi na Namba zinawakilishwa na Nukta 6. Pia kuna alama za Hisabati, Muziki, na Sayansi. Na hii hutumika Zaidi katika maofisi, vyuo na shule kwa ajili yakuwawezesha kufanya majukumu yao kama watu wengine.
Leave a Reply