Lyles ashangwazwa NBA kuitwa mabingwa wa dunia

Lyles ashangwazwa NBA kuitwa mabingwa wa dunia

Akiwa katika interview na waandishi wa habari baada ya ushindi wa medali ya dhahabu katika mashindano ya riadha nchini Marekani, mwanariadha Noah Lyles ameeleza juu ya ukosefu wa support kwa wanariadha nchi humo huku akishangazwa na mchezo wa mpira wa kikapu NBA kutambulika kama Mabingwa wa Dunia.

Aidha Mwanariadha huyo, ameshangazwa na kitendo cha washindi wa ‘Ligi’ ya mpira wa kikapu nchini Marekani, NBA kuitwa mabingwa wa dunia licha ya ‘Ligi’ hiyo kuchezwa katika ardhi ya Marekani pekee amesema.

Lyles  amesema, “Kitu kinachoniuma zaidi ni kwamba nikitazama Fainali za NBA, mshindi hutambulika kama bingwa wa dunia.

Bingwa wa dunia wa nini? Ninaipenda Marekani, lakini hiyo si dunia! Sisi (riadha) tuna wawakilishi karibu kila nchi kwenye mashindano haya, wakipeperusha bendera zao, Hakuna bendera katika NBA”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags