Lukamba: Zamaradi hakuna kitu kinaweza kukusumbua nikiwa hai

Lukamba: Zamaradi hakuna kitu kinaweza kukusumbua nikiwa hai

Aliyekuwa mpiga picha wa Diamond, Lukamba ameingilia kati maneno yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa kijana anayedai alikuwa akifanya kazi kwa Zamaradi lakini hakuwahi kulipwa ndani ya miezi 24 na anadai milioni 19.

Baada ya maneno hayo kuenea siku ya jana , Zamaradi uvumilivu ulimshida na kuamua kujibu tuhuma hizo ambazo limekuwa zikiendelea kwenye mitandao kwa kudai kuwa kijana huyo alikuwa ni mfanyakazi huru kwahiyo hakuwa na mkataba naye zaidi alikuwa akifanya kazi kwa siku.

Sasa basi kupitia hayo yote mwanamuziki na mpiga picha Lukamba amkingia kifua Zamaradi na kudai kuwa amewahi kufanya nae kazi na hawakuwahi kupishana hata kauli hivyo basi Lukamba amesemza hakuna atakayeweza kumsumbua Zamaradi kwenye upande wa production wakati yeye akiwa hai.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags