Luis afungiwa miaka mitatu

Luis afungiwa miaka mitatu

Rais wa zamani wa chama cha ‘Soka’ nchini Uhispania, #LuisRubiales amefungiwa kujihusisha na ‘soka’ kwa miaka mitatu.

Mwanzo Rais huyo alisimamishwa kujihusisha na ‘soka’ kwa siku 90 na FIFA ili kupisha uchunguzi kufuatia tukio la kumbusu mchezaji kwenye ‘fainali’ ya Kombe la Dunia la Wanawake nchini humo.

#Luis alimbusu mchezaji wa #Uhispania, #JenniHermoso mdomoni wakati wa hafla ya utoaji tuzo huko #Sydney Agosti 20, wakisherehekea ushindi wa bao 1-0 dhidi ya #England.

Rais huyo alijaribu kuendelea na majukumu yake kabla ya kulazimika kujiuzulu mwezi uliyopita, kufuatia tuhuma hizo, na hivi sasa ameadhibiwa baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka kifungu cha 13 cha kanuni za nidhamu za FIFA.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags