Ludacris: Jay-Z haniwezi kwenye kuandika mistari

Ludacris: Jay-Z haniwezi kwenye kuandika mistari

Mwigizaji na mwanamuziki kutoka Marekani Ludacris amedai kuwa msanii Jay-Z hamuwezi katika uandishi wa mistari ya nyimbo na endapo wangepewa masaa mawili ya kuandika basi yeye angeibuka kuwa mshindi.

Ludacris ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye podcast ya ‘Funky Friday’ ambapo ameeleza kuwa japo siku za hivi karibuni kumekuwa na ushindani mkubwa katika muziki wa Hip-Hop lakini anaamini kuwa Jay-Z hamuwezi katika uandishi wa verse.

Ikumbukwe kuwa Ludacris aliwahi kumshirikisha Jay-Z katika wimbo uitwao ‘I Do It for Hip Hop’ uliyopo kwenye albumu yake ya mwaka 2008 ya ‘Theatre of the Mind’.

Mkali huyo ambaye ameonekana katika filamu ya ‘Fast and Furious’ amekuwa akitamba na ngoma zake zikiwemo ‘Act a Fool’, ‘What’s Your Fantasy’, ‘Get Back’ huku akionekana katika filamu kama ‘Dashing Through the Snow’, ‘Crash’, ‘Hustle & Flow’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post