Liverpool yampata mrithi wa Klopp

Liverpool yampata mrithi wa Klopp

Klabu ya Liverpool ya England imefikia makubaliano na timu ya Feyenoord iliyo katika Ligi Kuu Uholanzi juu ya kumchukua kocha wa timu hiyo, Arne Slot kwa ajili ya kukiongoza kikosi hicho msimu ujao.

Kwa mujibu wa Sky Sport News imeeleza kuwa Slot anatarajia kuichukua mikoba ya kocha Jurgen Klopp ambaye ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu.

Slot mwenye umri wa miaka 45 ameiwezesha Feyenoord kutwaa taji la Ligi Kuu (Eredivisie) mwaka 2022 na mwaka huu kuchukua Kombe la Uholanzi huku ikiwa nafasi ya tatu hadi  sasa na pointi 75 nyuma ya vinara PSV yenye point 85.

Inaaminika kuwa aina ya ushambuliaji ya timu za Slot ni uwezo wake wa kuwakuza wachezaji ambapo ni moja kati ya mambo muhimu yaliyo mfanya kuwa chaguo la chaguo la kwanza la Liverpool kuanzia msimu ujao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags