Lil Wayne na The Rock wakataa sanamu zao

Lil Wayne na The Rock wakataa sanamu zao

Mwanamuziki wa Hi-hop kutoka nchini Marekani, #LilWayne inadaiwa kukataa muonekano wa sanamu lake ambalo lipo katika makumbusho ya #Wax mjini #Hollywood nchini humo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vinaeleza kuwa msanii huyo ameomba radhi makumbusho ya #Wax kuwa sanamu hilo halifanani na yeye, japo wamejaribu na anathamini juhudi zao.

 Ikumbukwe kuwa sanamu la ‘rapa’ huyo mwenye umri wa miaka 41 lilizinduliwa katika makumbusho hayo mwaka 2022.

Si huyo tuu muigizaji kutoka nchini humo #TheRock wiki iliyopita amedai kuongea na #Grevin iliyopo nchini #Ufaransa kuhusu marekebisho ya sanamu lake baada ya mashabiki kulikosoa sanamu hilo kwa kudai kuwa halifanani na muigizaji huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags