Lil Wayne kufunguliwa mashtaka

Lil Wayne kufunguliwa mashtaka

Ohooo!! Unaambiwa kimeumana bwana ambapo mlinzi wa zamani wa Rapper Lil Wayne yupo kwenye mipango ya kumfungulia mashtaka Boss wake huyo wa zamani,

Sasa bwana kwa mujibu wa TMZ mlinzi huyo anataka kufungua kesi hiyo baada ya Lil Wayne  kumtolea  bunduki wakati walipokua na mzozo nyumbani kwake mwezi uliopita

Hata hivyo ripoti ya zamani Lil Wayne anadaiwa kuingia kwenye ugomvi na mlinzi huyo baada ya kupiga Picha nyumba yake na kuzivujisha mitandaoni, jambo ambalo lilisababisha ugomvi huo kutokea.

Mwanzo mlinzi huyo hakutaka kumfungulia mashtaka  Lil Wayne na sasa amebadilisha mawazo na bado haijafahamika atamfungulia mashtaka gani msanii huyo, lakini kwa mujibu wa TMZ mlinzi huyo sasa anadai kuwa Lil Wayne alimpigia  kichwani na usoni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags