Leo siku ya bia duniani, mtaje rafiki yako ambaye unajua hakosi hii

Leo siku ya bia duniani, mtaje rafiki yako ambaye unajua hakosi hii

Wanywaji wa bia nchini Tanzania, leo Ijumaa Agosti 2, 2024 wanaungana na wenzao duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Bia inayolenga kuwaleta pamoja marafiki katika kufurahia ladha ya bia.

Siku ya Kimataifa huadhimishwa Ijumaa ya kwanza ya Agosti kila mwaka ambapo kwa mwaka huu imeangukia Agosti 2.

Maadhimisho ya siku hii yalianzia huko Santa Cruz, California nchini Marekani, mwaka 2007. Hadi sasa siku hii inasherehekewa katika miji 207 katika nchi 50 duniani zilizotawanyika katika mabara sita.

Lengo la kuanzishwa kwa kilevi hiki lilikuwa ni kuwaleta pamoja kufurahia ladha ya bia, kuwapongeza wanaozalisha bia na wanaohudumia pamoja na kuwaunganisha watu wa mataifa yote duniani kupitia kinywaji hiki pendwa.

Kila jamii duniani ina aina yake ya bia na historia inaonyesha kinywaji hiki kilianza kutengenezwa kisasa katika karne ya 18, hata hivyo, kabla ya hapo zilikuwepo pombe mbalimbali zilizokuwa zikitengenezwa kienyeji kutokana na teknolojia kuwa duni.

Tanzania pia ina wanywaji wengi wa bia ambao kuanzia siku za mwisho wa wiki kama Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, wanakusanyika kwenye baa mbalimbali na kujumuika na watu tofauti.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post