Leo dunia inaadhimisha siku ya kula unachokitaka

Leo dunia inaadhimisha siku ya kula unachokitaka


Kila ifikapo tarehe ya leo Mei 11, ulimwengu unaadhimisha siku ya kula unachokitaka duniani.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘National Day Calendar’ imeeleza namna siku hii inavyo sheherekewa ambapo unaweza kupika au kuandaa chakula unachokipenda na ukala pia unaweza kupigia marafiki na kwenda kwenye mgahawa na kupata chakula na burudani.

Siku hii imeundwa na Thomas na Ruth Roy wa ‘wellcat.com’, ‘Siku ya Kula Unachotaka’ ambapo hata wale waliyoko kwenye diet wanaweza kuchukuwa mapumziko kwa leo kwani hata wataalumu wanakubali kuwa kupumzika siku moja ni nzuri kwa afya yako.

Vipi ungependa kula nini siku ya leo?


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post