Lamar amjibu Drake

Lamar amjibu Drake

Baada ya ukimya wa wiki kadhaa ‘rapa’ kutoka nchini Marekani Kendrick Lamar amerudi tena mjini akiwa na ngoma mpya ambayo ameitoa kwa ajili ya kumjibu Drake.

Ngoma hiyo iliyotoka siku wa jana iitwayo ‘Euphoria’ tayari imeonekana kuwa ngoma kubwa nchini humo baada ya kuingia namba one trending katika mtandao wa YouTube ikiwa ni saa chache tuu tangu kuachiwa kwake.

Lamar amemjibu ‘rapa’ huyo baada ya Drake wiki iliyopita kuachia wimbo wa ‘Taylor Made Freestyle’ aliyotumia AI (akili bandia) kutengeneza sauti ya marehemu Tupac.

Lakini wimbo huo wa Drake umefutwa baada ya mwanasheria wa familia ya Tupac, Howard King kudai kuwa ilikuwa siyo uungwani kutumia sauti ya marehemu bila idhini ya familia yake huku wakili huyo akimtaka Drake kufuta wimbo huo ndani ya saa 24.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags