Kylie Jenner alia na wanaonanga mwonekano wake

Kylie Jenner alia na wanaonanga mwonekano wake

Mfanyabiashara kutoka Marekani Kylie Jenner aangua kilio kutokana na mashabiki kuunanga mwonekano wake wa sasa baada ya kufanya surgery.

Kylie ameeleza maumivu anayoyapitia katika onesho la ‘Reality Show’ ya The Kardashians, katika kipande kilichooneshwa jana Juni 20 akiwa anaongea na dada yake Kendall Jenner kwa kueleza kuwa maneno mabaya kutoka kwa watu mitandaoni yanamuathiri sana.

“Nilienda safari mwaka jana kwa ajili ya kujaza lipsi za midomo yangu, lakini ilikuwa tofauti baada ya kuanika muonekano wangu, kwa nini watu wanadhani ni sawa kuzungumza kunihusu? Sijawahi kulia kuhusu hili hapo awali, lakini nadhani linaniathiri” alisema huku akitokwa na machozi

Ikumbukwe kuwa mapema mwaka huu Kylie Jenner alitengeneza vichwa vya habari kuhusu mwonekano wake mpya baada ya kupiga picha wakati wa wiki ya mitindo Paris lakini jambo hilo lilikuwa tofauti kwa mashabiki wakidai kuwa surgery ilienda vibaya na kuwa anaonekana kama mzee.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags