Kyle Walker na mkewe kusuluhisha matatizo yao

Kyle Walker na mkewe kusuluhisha matatizo yao

Baada ya kutokuwa kwenye maelewano kwa muda wa miezi mitano mchezaji wa ‘klabu’ ya #ManchesterCity, #KyleWalker na mkewe #AnnieKilner wameonekana kuwa katika hatua ya kurudisha mahusiano yao.

Kwa mujibu wa Tmz News imeeleza kuwa huwenda beki huyo na mkewe wanampango wa kusuluhisha matatizo yao baada ya kuonekana pamoja katika sherehe iliyofanyika kwenye Jumba la Wyne na Coleen mjini #Cheshire nchini Uingereza.

Hata hivyo siku za hivi karibuni wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwa na watoto wao ambapo imedaiwa kuwa huwenda wapo katika hatua ya kuiweka sawa familia yao kama ilivyo kuwa awali.

Januari 12 mwaka huu wanandoa hao walikuwa na ugomvi mkubwa wa wivu wa kimapenzi ambapo Walker alidaiwa kuwa na mtoto mwingine aliyezaa na mwanamke aitwaye #LaurynGoodman.

Ikumbukwe kuwa wawili hao walidumu katika mahusiano yao ya uchumba kwa miaka 12 ambapo walifunga ndoa mwaka 2022 na wamebahatika kupata watoto wa nne.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags