Kuwa na mwandiko mbaya ni ulemavu

Kuwa na mwandiko mbaya ni ulemavu


Dysgraphia ni ugonjwa wa neva za binadamu kupata shida kugeuza mawazo yake kuwa katika maumbo mazuri ya kiuandishi ambayo wengi huita mwandiko mbaya.

Wataalamu wanatafsiri hali hii kama ulemavu wa kushindwa kujieleza kwa maandishi. Watu wenye dysgraphia wanatajwa kuandika polepole kuliko watu wengine.

Aidha suala la mwandiko mbaya haliusishwi na uwezo mdogo wa darasani, badala yake wengi wenye tatizo hili huwa na uwezo mzuri wa kufikiri, lakini ugumu wanapata kwenye kuunda herufi wanapoandika.

Hata hivyo watu wenye dysgraphia wanauwezo wa kupata usaidizi na kuondokana na tatizo hilo kutoka kwenye familia zao na shuleni kwa kuandaliwa masomo maalumu ya kuumba herufi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags