Kuwa makini na utapeli wa aina hii chuoni

Kuwa makini na utapeli wa aina hii chuoni

Na Michael Onesha
Niaje niaje watu wangu wa nguvu, leo ndani ya unicorner nimekusogezea mada ambayo inakuamsha wewe mwanafunzi wa chuo ambaye bado umeamua kukumbatia matatizo yanayoweza kusababisha usifanikiwe kumaliza hata hicho chuo chenyewe.

Baadhi ya wanafunzi ukiwaambia ukweli wanaona kama unawaonea lakini leo tunarudia tena kuwajuza, ni asilimia chache za mahusiano yanayoanzia chuoni na kufikia hadi ndoa hivyo basi epuka kudanganywa kudanganyika na mahusiano ya chuoni.

Chuoni ni sehemu ya kupata elimu na njia ya jinsi gani unaweza kujikwamua kimaisha lakini baadhi ya wanafunzi wamegeuza sehemu hiyo kufanyia utapeli wa mapenzi huku changamoto hiyo ikitajwa kuendelea kushamiri siku hadi siku.

Inajulikana kuwa mahusiano ya kimapenzi hayaepukiki sehemu yoyote lakini ukiwa kama mwanachuo unatakiwa kuyaepuka mambo haya ili usiingie kwenye dimbwi la utapeli wa mahusiano chuoni.

• Kukubali kuzaa na mtu ili upate ndoa
Moja ya utapeli ambao wanafunzi na wadada wengi wamekuwa wakiangukia ni mpenzi kukuomba umzalie kabla ya ndoa, wewe msichana au binti kumbuka ukishabeba ujauzito ndoto zako zinabidi zisubiri mpaka pale utakapojifungua , fuata kilicho kupeleka chuoni achana na vishawishi hivi.

• Kumsomesha mpenzi
Jambo la pili ambalo vijana wengi huwa wanashawishika nalo ni kuwasomesha wapenzi wao au kuwasaidia maisha ya chuoni kwa kutumia pesa za boom wakitegemea anayemlipia hizo pesa aje amuoe hapo baadaye, dunia kwa sasa imebadilika siku hizi hadi baadhi ya wanawake ni matapeli so wewe kijana kama ulikuwa na mpango wa kufanya hili basi acha mara moja.

• Marafiki
Ukiwa kama mwanafunzi wa chuo ambaye ndiyo umeingia au unaendelea na chuo, jambo ambalo unatakiwa kulizingatia ni kuepukana na watu wanaoitwa marafiki, rafiki ndiye mtu ambaye atakupeleka kwenye mafanikio vile vile atakaye kupeleka kwenye shida.

Baadhi ya wanachuo wengi wamekuwa wakifeli maisha kutokana na kuwasikiliza marafiki na mashosti wao, kijana zinduka umefuata chuo kusoma na familia yako inakutengemea unachotakiwa kukifanya ni kufuata kilicho kupeleka chuoni na si vinginevyo.

Marafiki ndiyo watu watakao kubadilisha kuanzia, maisha, mtindo wa mavazi, so akili kichwani mwako waswahili wanasema ‘Akili za kuambiwa changanya na zako’.

• Mahusiano chuoni
Mahusiano ni jambo ambalo halikatazwi mtu lakini, ukiwa kama mwanafunzi kuanzisha mahusiano ukiwa chuo kunaweza kukufanya ukapoteza muelekeo wa maisha yako, mahusiano mengi ya chuo ni ngumu kukuta yametoboa ni machache sana hii ni kwa sababu ya kukutana kwa msimu, mmoja aendapo likizo na mapenzi yameisha mkirudi chuo yanarudi tena hii ndiyo aina ya mahusiano chuoni jitahidi sana usiingie katika mtego huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post