Kusah: Unaweza kutoboa bila kuwa kwenye lebo kubwa

Kusah: Unaweza Kutoboa Bila Kuwa Kwenye Lebo Kubwa

 Weeeeeeh! Unaambiwa ndo kwanza kumekucha watu wanajisifia kuwa kizuri ndo kinapendwa sio lazima kiwe kimefanyika katika lebo inayo julikana, maneno hayo bwana kayaandikwa na  mwamba Kusah baada ya kufikisha watazamaji million 10 kwenye wimbo wake wa “I wish”

Kusah amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa “zilikuwa ndoto zangu za kila siku hatimae Mungu ametenda na kunifundisha kwamba kila kitu kinawezekana, kwa upande wangu hili ni kubwa sana million 10 viwes in 9 months, wengi wanadhani kwamba huwezi kufika kokote bila kuwa chini ya Boss, Lebo na watu wenye nguvu kubwa kwasasa imekuwa tofauti kizuri ndo hupendwa” ameandika Kusah

Aidha aliendelea kwa kuandika kuwa “ wadogo zangu, kaka na dada zangu ambao ndio kwanza mmeingia kwenye industry niwaambie tu kwamba nafasi ni nyingi na kila kitu kinawezekana ukiamini, nakumalizia asanteni sana watu wangu” ameandika Kusah

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post