KUSAH: Nimeumizwa sana kwenye mapenzi

KUSAH: Nimeumizwa sana kwenye mapenzi

Na Habiba Mohamed

Mambo vipi mtu wangu wa nguvu. It's another time nakusogezea habari zinazohusu mastaa wako uweze kuburudika na kujifunza. Ebwanaa yule mkalii wa tungo za malavidavi, Baba Nono maarufu kama Kusah amefunguka na kusema ameumizwa sana kwenye mapenzi.

Msanii huyo amefunguka  kwamba ameumizwa sana kwenye mapenzi na kusababisha yeye kuanza kuandika mashairi ya mapenzi, pia alikiri kuwa yeye anapenda kupendwa.

"Napenda kupendwa sana, nishaumizwa sana na mapenzi ndo imenifanya niandike mashairi yangu kuhusu mapenzi pia nimegundua mashabiki zangu wanavutiwa na nyimbo za mapenzi hivyo inanifanya niongeze juhudi katika utunzi wa nyimbo hizo," alisema Kusah.

Vilevile aliongezea kusema "Idadi kubwa ya mashabiki zangu ni wanawake kutokana na nyimbo ninazoimba, imenisaidia kupata jina kwaajili ya EP yangu. Aidha, kazi yangu imeniongezea mapenzi kwa mzazi mwenzangu (Aunty Ezekiel) ambaye ananipa nguvu ya kupambana maana kazi zangu zinambembeleza."

Akamalizia kusema, "Sichoki kuandika nyimbo za mapenzi maana zinanifanya nifurahie kazi zangu, mapenzi ni maisha ingawa ni kitu kinachoumiza zaidi mashabiki zangu wategemee mziki mzuri kwenye EP yangu na kazi zijazo."

Alooooh! Aya bhana wale wenzangu na mie hasira zetu za kuumizwa kwenye mahusiano, maumivu unayatibu vipi au ndo tukuache kidogo hayatuhusu.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post