Kunguni wazua balaa Ufaransa

Kunguni wazua balaa Ufaransa

Wakazi wa Paris nchini Ufaransa wajikuta wakiingia kwenye mapambano dhidi ya kunguni ambao wamekuwa wakienea katika maeneo mbalimbali.

Inaelezwa kuwa mwazo kunguni hao walikuwa wakionekana katika mahoteni, vyumba vya kukodisha na kwenye kumbi za kuangalia sinema, lakini kwa sasa imekuwa tofauti kwani ongezeko la wadudu hao limekuwa kubwa.

Hawajaishia hapo tu bali wamehamia hadi kwenye ‘treni’ za kusafirishia abiria kwenda kwenye maeneo mbalimbali, huku hofu kubwa kwa wananachi ni kuhamishia waduduhao nyumbani

Hata hivyo si mara ya kwanza kwa Ufaransa kukumbana na wadudu hao kwani miaka mitatu iliyopita serikali ya Ufaransa ilizindua kampeni ya kupambana na kunguni, ambayo walitoa namba ya simu ya mawasiliano kwa ajili ya kutoa taaifa za maeneo yenye wadudu hao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags