Kuanzia leo, Mwiko wanafunzi kutumia simu shuleni australia

Kuanzia leo, Mwiko wanafunzi kutumia simu shuleni australia

Simu zapigwa marufuku kwa wanafunzi katika shule za serikali nchini Australia wakati wa saa za shule au wakiwa darasani.

Hiyo ni kutokana na kuepusha usumbufu darasani wakati wa vipindi vya masomo vinapoendelea.

Shule zote za Sekondari zilizo chini ya serikali nchini humo na shule za msingi zinatakiwa  kutekeleza amri hiyo kuanzia leo, isipokuwa kwa wanafunzi wenye matatizo ya kiafya, kama vile kuangalia  kiwango cha sukari kupitia application za simu.

Waziri wa Elimu, Prue Car amesema kuwa kila shule imekuwa ikishauriana na idara yake ili kutekeleza agizo hilo, kwa kuchukua simu hizo na kuzizima kisha kuzihifadhi katika ulizi wa shule ili kuboresha matokeo ya anafunzi.

Hapo awali wanafunzi walikuwa wakitumia simu kwa kufanyia kazi za shule hali iliyopelekea matokea mabaya mashuleni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post