Kuachana kwa Cardi B na Offset hakuzuii watoto kufurahi

Kuachana kwa Cardi B na Offset hakuzuii watoto kufurahi


Mwanamuziki wa Marekani Cardi B na mumewe Offset wameripotiwa kuonekana pamoja wakifurahia siku ya kuzaliwa ya mtoto wao siku chache zilizopita licha ya wawili hao kuwasilisha ombi la talaka mahakamani.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tmz inaeleza kuwa mchakato wa talaka ya Cardi na Offset bado unaendelea huku wakidaiwa kuingia kwenye makubaliano ya kuwa marafiki kwa ajili ya maendeleo ya watoto wao.

Utakumbuka kuwa miezi kadhaa iliyopita Cardi aliwasilisha ombi la talaka mahakamani ikiwa ni baada ya kusambaa kwa picha za Offset mitandaoni zikimuonesha akiwa kwenye huba zito na mpenzi wake wa zamani.

Mbali na kuwasilisha talaka hiyo pia Cardi alitangaza kuwa na ujauzito huku akimtaja Offset kuwa ndiye mwenye ujauzito huo, hata hivyo Cardi alifunguka kuwa ujauzito huo haumzuii yeye kuendelea na mchakato wa talaka.

Wawili hao walifunga ndoa Septemba 20, 2017, na hii siyo mara ya kwanza kwa Cardi kudai talaka kwani mwishoni mwa mwaka jana alidai talaka lakini baada ya mwezi mmoja kupita wawili hao walirudiana tena.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags