Kope bandia zilivyomtesa muuguzi Valeria

Kope bandia zilivyomtesa muuguzi Valeria

Akiwa mpenzi mkubwa wa kuongeza kope bandia kwa karibu mwaka mzima, muuguzi wa Brazili Valéria Campos hakuwahi kufikiria kwamba angeweza kupata aina fulani ya mzio wakati wa kufanya upasuaji. 

Hata hivyo, miezi minne baada ya kudumu na kope bandia  aliporudi saluni kuweka kope zingine baada ya zile za awali kuonekana kuanguka muda unavyokwenda aligundua kuwa kuna kitu hakiko sawa. 

Muuguzi huyo anaripoti kwamba saa tatu baada ya zoezi hilo, jicho lake likaanza kuwa jekundu, kuvimba, na kupata maumivu. 

 "Mtaalamu huyo alitumia njia zile zile ambazo tayari nilikuwa nimezizoea. Lakini kadiri saa zilivyopita, jicho langu lilivimba na kuumia zaidi na zaidi," amesema Valéria.

Baada ya kuziondoa, alienda kwenye chumba cha dharura cha hospitali ya Belo Horizonte, Brazili, ambako alipewa rufaa ya kupata huduma ya dharura ya macho.

"Kwa kweli sikuweza kulala usiku huo, ilikuwa saa 3 asubuhi nilipoamka na sikuweza kufungua macho yangu tena. Kwa mujibu wa daktari, nilikuwa na maambukizi, lakini sikujua kama yalitokana na kope za 'syntetisk' au gundi iliyotumiwa." Aliongeza. 

ili kupona kabisa kutokana na maambukizi, Valéria alihitaji antibiotics kwa siku saba, Ingawa tatizo hilo halikuathiri uwezo wake wa kuona hata kidogo, anasema kope zake za asili hazikua tena au kuwa na wingi uliokuwa nao kabla ya kuongezwa muda. "Idadi ya kope nilizonazo zimepungua kwa sababu nilikuwa na nywele nyingi za asili," anahitimisha.

kope bandia za syntetisk

Katika kuboresha urembo wake, Mwanafunzi wa saikolojia Adne Lucilla Carvalho Santos aliamua kuweka kope bandia za nyuzi za syntetisk kwa mara ya kwanza mnamo Julai.

'Jambo ambalo sikutarajia ni kwamba ningepatwa na mzio'.

Dakika chache baada ya kumaliza kuweka, mwanafunzi wa chuo kikuu anakumbuka kwamba alianza kuhisi usumbufu machoni pake. Dalili za kwanza za maambukizi ni uwekundu na na macho kama kuchomachoma. Kitu cheupe kinaonekana kwenye jicho la Adne, ni kama jeraha

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags