Kongamano  la data kuanza rasmi desemba 6

Kongamano la data kuanza rasmi desemba 6

Eeh bwana eeh!!  moja kati ya stori ambayo inakuhusu wewe kijana na mdau wa mwananchi scoop ni hii hapa ambapo Taasisi ya Tanzania Data lab(dlab) kwa kushirikiana Mwananchi Communications Limited (MCL) pamoja na wadau mbalimbali wameandaa kongamano la kujadili umuhimu wa data katika ukuzaji wa uchumi kidijitali.

Kama kijana taarifa hii inakuhusu sana ambapo, Mkurugenzi Mtendaji wa dlab, Stephen Chacha amesema kongamano hilo la tatu litafanyika kuanzia Desemba 6 hadi 8 mwaka huu  likikutanisha zaidi ya watu1000 watakaoshiriki kwa njia ya ana kwa ana huku wengine kwa mtandao.

 “Katika Tamasha hilo kutakua na wadau mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, kilimo, biashara,jinsia, kazi, usimamizi wa data, majisafi, mazingira, mabadiliko ya tabia ya nchi, utawala, uwajibikaji na waandishi wa habari watakaa pamoja na kutathmini umuhimu wa data katika uchumi wa kidijitali”alisema Chacha

Hata hivyo Mkuu wa Kitengo cha Digital wa MCL ambao ni wazalishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti  pamoja na chaneli ya Youtube ya Mwananchi Digital, Mihayo Wilmore amesema kampuni hiyo itajikita zaidi katika kueleza uzoefu wake katika matumizi ya data kwa uhabarishaji pamoja na kuhabarisha umma juu ya tukio hilo.

“Katika kongamano hilo kutakuwa na mdahalo kuhusu data na habari, na kampuni yetu (MCL) inahusika na habari na imekua kituo cha watu kujiridhisha na taarifa wanazozipata kwingine” alisema Mihayo.

Ebwana eeh!!! Ukisikia komaaa na fursa ndo hii sasa ni wakati wako kijana kufuatilia kongamano hili unaweza ukapishana na gari la mshahara bwana zingatia hiyo!!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags