Konde Boy bado kuna shida

Konde Boy bado kuna shida

Anaandika sana. Sioni mwenye uwezo huo kwa kizazi hiki. Anaandika mpaka kuandika kunamshangaa. Msikilize kwenye “Bakhressa”, “Kama Unamjua” ama rudi kwenye mipini yake akiwa bado ananata na ‘biti’ za ‘Usafini’.

Siyo kuandika tu, hata ‘melodi’ na uwezo wa visa vya kuandikia, yupo kwenye utawala wa peke yake.Konde Boy, licha ya ubora wake. Bado napata shaka na usimamizi wake.

Uwezo wa kuandika na ubora wa kubuni ‘melodi’ unapaswa usindikizwe na timu nzuri ya usimamizi wa kazi na maisha binafsi. Nje ya hapo simuoni. Bado sijaona mabadiliko kwenye eneo hili. Na kimsingi hapa anaachwa gepu kubwa na kaka yake wa ‘’Usafini’. Ila kwenye mipini dogo kama upepo wa moto.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags