Komasava ya Mondi yamfikia Swae Lee

Komasava ya Mondi yamfikia Swae Lee

Wimbo wa mwanamuziki Diamond Platnumz wa ‘Komasava’ aliomshirikisha Chley na Khalil Harrison umeendelea kuupiga mwingi na sasa umemfikia ‘rapa’ wa Marekani Swae Lee ambaye alionekana akisikiliza wimbo huo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Diamond ame-share video hiyo ikimuonesha mwanamuziki huyo wa Marekani akicheza wimbo huo ambao mpaka kufikia sasa una zaidi ya watazamaji milioni 2.4 kupitia mtandao wa YouTube.

Utakumbuka kuwa wiki chache zilizopita kupitia mtandao maarufu wa Burudani, Afrika Kusini wa ‘Culture Collecter’ uliuliza swali kuhusiana na wimbo kutumika katika michuano ya Kombe la Dunian 2026.

Aidha kwa mujibu wa baadhi ya wadau mbalimbali walijitokeza katika upande wa ‘komenti’ wakionekana kukubaliana na wazo hilo kutokana na wimbo huo kutaja Lugha za nchi mbalimbali na kufanya ngoma hiyo kuwa kubwa duniani kote.

Hata hivyo shabiki mmoja aitwaye ‘__capitano10’ aliitoa alama 10/10 kwenye wimbo huo.

“Una uwezo wote wa kuwa wimbo wa theme wa Worldcup 2026 kupitia kipande kilichobobea vizuri kilichoratibiwa na mkali wa muziki Diamond Platnumz ambayo inatoa vibes ya furaha na tune ya kucheza. naipa 10/10”.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags